Skip to content

Sauti Sol – Nenda Lote Lyrics

Nenda Lote By Sauti Sol

Umetuma wazazi wako waje wanielezee
Umetuma wazazi wako waje wanielezee
Hunitaki tena
Na mashoga zako waje waniambie
Na mashoga zako waje waniambie
Ndoa tumeivunja

Siamini Kuna time singeishi bila wewe
Mapenzi ya kukata na shoka eeh
Yashamwagika hayazoleki haya oh
Basi nenda lote mama
Nenda lote mama

Mpenzi unaenda
Nilikuenzi kinomanoma
Yashamwagika hayazoleki haya oh
Nenda lote mama

Ukatuma lawyer wako aje anisomee
Ukatuma lawyer wako aje anisomee
Kuwa watoto ulionizalia eeh
Kuwa watoto ulionizalia eeh
Sitawaona tena

Siamini kuna time tuliapa hadharani
Kanisani kwa Chanda na Pete eeh
Yashamwagika hayazoleki haya oh
Nenda lote mama
Nenda lote mama

Mpenzi unaenda
Nilikuenzi kinomanoma
Yashamwagika hayazoleki haya oh
Nenda lote mama

Ukatuma pastor wako aje anikemee
Ukatuma pastor wako aje anikemee mama
Na madeni zangu ukazitangaza eeh
Na madeni zangu ukazitangaza eeh
Mitandaoni

Shemeji zangu ndugu zako tukionana
Wambie sisi bado rafiki eeh
Wasinipite barabarani mama oh
Umeenda lote mama
Umeenda lote mama

Mpenzi unaenda
Nilikuenzi kinomanoma
Yashamwagika hayazoleki haya oh
Basi nenda lote mama
Nenda lote mama

Mpenzi unaenda
Nilikuenzi kinomanoma
Yashamwagika hayazoleki haya oh
Nenda lote mama
Mama, mama
Nenda lote mama